John 20:11-16

11 aLakini Maria Magdalene akasimama nje ya kaburi akilia. Alipokuwa akilia, akainama, kuchungulia mle kaburini, 12 bnaye akaona malaika wawili wamevaa mavazi meupe, wameketi pale mwili wa Isa ulipokuwa umelazwa, mmoja upande wa kichwani na mwingine upande wa miguuni.

13 cWakamuuliza Maria, “Mwanamke, mbona unalia?”

Akawaambia, “Nalia kwa kuwa wamemchukua Bwana wangu na sijui walikomweka.”
14 dBaada ya kusema hayo, akageuka, akamwona Isa amesimama, lakini hakumtambua.

15 eIsa akamwambia, “Mwanamke, mbona unalia? Unamtafuta nani?”

Maria akidhani ya kuwa aliyekuwa anaongea naye ni mtunza bustani, kwa hiyo akamwambia, “Bwana, kama ni wewe umemchukua, tafadhali nionyeshe ulikomweka, nami nitamchukua.”

16 fIsa akamwita, “Maria!”

Ndipo Maria akamgeukia Isa na kusema naye kwa Kiebrania, “Rabboni!” (Maana yake Mwalimu).

Copyright information for SwhKC